WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
|
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
S. L. P. 1509,
DODOMA.
29 Aprili, 2019
|
|
|
Simu Nambari: +255-22-2113537
Telefax: + 255-22-2184569
Barua Pepe: fire.rescue@frf.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI
AFANYA MABADILIKO YA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA
Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, (CGF) Thobias Andengenye, amefanya
mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa hapa nchini.
Makamanda walioguswa
na mabadiliko hayo ni Kamishna Msaidizi wa Zimamoto (ACF) Mohamed Kondo, aliyekuwa
Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni, anaenda kuwa Kamanda wa
Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya.
Kamishna Msaidizi
(ACF) Juma Yange, aliyekuwa Kitengo cha Utawala Mkoa wa Kinondoni, anakuwa Kamanda
wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kizimamoto Kinondoni.
Mrakibu Msaidizi wa
Zimamoto (ASF) John Francis, aliyekuwa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Handeni
Mkoani Tanga, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Rukwa.
Vilevile, aliyekuwa
Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto
(ASF) Athumani Basuka, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Hai
– Siha, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Jumbe Juma.
Pia aliyekuwa
Kamanda wa Kiwanja cha Ndege Mkoa wa Iringa, Mkaguzi wa Zimamoto (INSP) Hamisi
Dawa, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera.
Mabadiliko haya ni
ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika kuongeza
ufanisi wa utendaji kazi.
Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji linaendelea kutoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Makamanda
wa Zimamoto na Uokoaji Mikoa na Wilaya katika suala la Kinga na Tahadhari Dhidi
ya majanga.
Imetolewa
na;
Joseph Mwasabeja –
(INSP)
Msemaji wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji
Makao Makuu.