Na Mwandishi wetu , Mbeya
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia
na Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako leo ametembelea na kukagua hatua za
maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe
Kampasi ya Mbeya, ambapo amepongeza Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa hatua za ujenzi
ulipofikia.
Akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa
Chuo hicho Pro. Lughano Kusiluka, Prof Ndalichako amemwelekeza Mkandarasi wa
Ujenzi kuhakikisha kufikia Juni 2019
ujenzi wa Jengo hilo kuwa umekamilika kama ilivyopangwa.
Kukamilika kwa ujenzi kutawezesha
jumla ya wanafunzi 900 kupata vyumba vya madarasa mbali na kumbi za mikutano na
ofisi za uendeshaji. Jengo hilo
linatarajiwa kuwekwa jiwe la Msingi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Joseph Magufuli Mei 1, 2019.
Mhe. Waziri Ndalichako akiongozwa na Mkandarasi
wa mradi akikagua vyuma vya madarasa mara
alipowasili kukagua ujenzi wa jengo la
ghorofa tano la Taaluma na Utawala linalotazamiwa kumalizika mwezi Juni,2019. Pamoja
naye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka, Naibu Mawakamu
Mkuu wa Chuo Utawala na fedha Prof. Ernest Kihanga na wasimamizi wa ujenzi
Mhe. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiweka saini kwenye kitabu cha wageni kwenye eneo la ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya mbeya mara tu baada ya kuwasili. Aliyeshika kitabu ni Injiani Thadeus Koyanga na kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka ( Mwenye Kaunda suti kushoto)
Mhe. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (kushoto) akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka ( Mwenye Kaunda suti kushoto) pamoja na Mkandararasi na wajenzi; wakikagua ramani ya jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya.
Mhe. Profesa Ndalichako (katIkati) akikagua
mahali litakapojengwa jiwe la msingi ambalo litawekwa rasmi na Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muuungano wa
Tanzania Dr.John Pombe Joseph Magufuli Mei 1, 2019. Kushoto ni Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka na kulia ni Mkadarasi wa Ujenzi
Injinia Thedeus Koyanga (mwenye shati la mikono mirefu) akifuatiwa na Profesa Ernest Kihanga Naibu Makamu Mkuu wa
Chuo Utawala na Fedha.
Mhe. Profesa Joyce Ndalichako alikagua
muonekano wa nje wa jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya
Mbeya pamoja na kukagua usafi wa mazingira, alipofanya ziara ya kukagua
maendeleo ya ujenzi kabla Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli hajafika kuweka
jiwe la msingi.