Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania umesema katika kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kukuza Demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari Umetenga shilingi millioni 500 zitakazo wezesha vyombo vya habari na waandishi wa habari nchini kufanya tafiti na kuandika Habari zinazoelimisha jamii
Hayo yamesemwa na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Michael Battle katika kongamano la kitaifa la Sheria za vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza lililoanda liwa na shirika la haki za binadamu THRDC juni 27,2024 jijini Dar es salaam
Aidha Battle Ameipongeza serikali ya Rais Samia Suluhu kwa kuruhusu uhuru kwa vyombo vya habari na kwamba hata hivyo bado haitoshi kusema kwamba kuna uhuru kamili na kwamba kunaulazima wa kiboresha hali ili kuondoa vitisho kwa waandishi wa habari ili wawe huru zaidi kufanya kazi yao.
.jpeg)