MUHIMBILI KUMUAMISHIA MARIAMU RAJABU HOSPITALI YA SARATANI OCEAN ROAD

 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Jopo la Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili lililokuwa likimfanyia Uchunguzi Mwanadada Mariamu Rajabu kwenye kidonda chake cha Mgongoni limekubalina kwa pampja kumuamishia mgonjwa huyo katika Tasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam.

akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ibrahim Mkoma amesema kuwa mara baada ya jopo la madaktari wa Hospitali ya Tiafa Muhimbili kufanya uchunguzi kwa kina na wameamua kumpa rufani mgonjwa huyo kwenda Ocean Roan hili aweze kupata matibabu zaidi.

hata hivyo waandishi wa habari walipohoji nini matokeo ya uchunguzi wa na kwanini wanamuamishia katika Hospitali ya Saratani Dk Mkoma alikataa kutoa taharifa ya matokeo ya uchunguzi wake na kusema kuwa matokeo hayo ya ugonjwa huo ni siri ya Daktari na Mgonjwa kwa kama kanuni za kitabibu zinavyohitaji.

hata hivyo globu ya jamii ilipomuuliza Mariamu Rajabu juu ya ugonjwa wake alisema kuwa awezi kuzungumzia ugonjwa huo kwa sasa na ayupo tayari kuzungumzia ugonjwa wake.

Muhimbili (MNH) ilianza  kumfanyia uchunguzi Mariam Rajab kubaini chanzo cha kidonda alicho nacho mgongoni. Taarifa za ugonjwa wa Mariam zilisambaa siku chache zilizopita kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha binti huyo akiomba msaada wa matibabu kufuatia kidonda hicho kilichodumu kwa muda mrefu.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha alizungumza na waandishi wa habari  Alhamisi Aprili 18,2019 amesema hospitali hiyo imechukua jukumu la kumtibia Mariam baada ya kupata maelekezo kutoka wizara ya afya na serikali itabeba gharama zote.

 alisema waliona ile video nakufanya juhudi za kumtafuta na hatimaye ametoka Singida na kukaa naye wodini, kwa  matibabu  yanaendelea na tayari madaktari wamechukua vipimo kwa ajili ya uchunguzi zaidi,

 Mariam alieleza kuwa kidonda hicho amekuwa nacho kwa muda mrefu na amekuwa akikitibia mara kwa mara ila Agosti 2018 kimefuka upya na kumsababishia maumivu makali. 24/04/2019

  Mkuu wa idara ya upasuaji MNH, Ibrahim Mkoma amesema matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa ndiyo yatakayotoa mwongozo ni aina gani ya matibabu ambayo Mariam anatakiwa kupatiw

 Mwanadada Mariamu Rajabu  akiwa amelala kwenye kitanda akisaidiwa  na muhudumu wa afya wa hospitali ya Tiafa Muhimbili.
Jopo la Madaktari walikuwa wakimuhudumia Mwanadada Mariamu Rajabu  akiwa amelala kwenye kitanda  hospitali ya Tiafa Muhimbili.

Post a Comment

Previous Post Next Post