Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii
Wito
umetolewa kwa Wanawake wanaofanya shughuli za uvuvi na kuchakata mazao ya uvuvi
kutumia chama chao kuweza kupanua fursa ya masoko baina ya wao kwa wao kutokana
na sehemu wanazotoka.
Hayo
yamesemwa leo April 15 jijini Dar es Salaam 2019 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha TAWFA
Kilichofanyika katika Hotel ya Mbezi Garden Jijini Dar es Salaam.
“TAWFA ni
mtandao au chombo kitakachotumika kuwaunganisha kwa pamoja Wanawake wote
wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi hapa nchini ,pia kupitia TAWFA,nataraji
kwamba wanawake watatoa changamoto na uzoefu wao kwa sauti moja katika shughuli
za uvuvi na kuuza mazao ya uvuvi”amesema Dk . Rashid.
Amesema kuwa
TAWFA Ndio chombo pekee kutoka Tanzania kitakachokuwa mwanachama katika mtandao
wa Africa (Africa Women fish processors and Traders Association-AWFISHNET)
Ambao umeunganisha wanawake wote Africa wanaojishughulisha na uchakataji na
biashara ya samaki na mazao yake ili wawe na sauti moja katika kushiriki kwenye
masuala mbalimbali.
Pia alitoa
wito kwa wanawake wote wanaohusika katika mtandao wa TAWFA waweze
kushirikiana,kupendana na kusaidiana katika shughuli zenu ili kuwa na uelewano
wa kibiashara na kukuza kipato na uchumi kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wanawake wanaojishughulisha kuchakata mazo ya Uvuvi nchini(TAWFA) Wakati wa hafala ya ufunguzi wa Chama hicho Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Chama cha Wanawake wanaojishughulisha na kuchakata mazo ya uvuvi nchini
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Emedo akizungumza mbele ya mgeni rasmi kumeuleza mchakato wa kuanzishwa kwa TAWFA
Sehemu ya Wanachama wa TAWFA Walioshiriki uzinduzi wa chama chao jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama akikagua baadhi ya mazo ya uvuvi yalionyeshwa na Wanawake hao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama akikagua baadhi ya mazo ya uvuvi yalionyeshwa na Wanawake hao.
Sehemu ya Wanachama wa TAWFA Walioshiriki uzinduzi wa chama chao jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa TAWFA.