WANAFUNZI 200 KUSHIRIKI MASHINDANO YA WANASAYANSI CHIPUKIZI 2019

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Jumla ya Wanafunzi wapatao 200 wanataraji kushiriki katika maonyesho ya wanasayansi Vijana yatakayofanyika nchini kuanzia tarehe 31 julai 2019.

akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaame Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Tasisi ya Tanzania Young Scientist(YST), Dr. Gozbert Kamugisha  amesema kuwa Maonyesho ya YST 2019 yatachagua wanafunzi 200 wenye kiwango bora  amabo wamefanya tafiti zenye tija katika jamii.

"tafiti za kisayansi na teknolojia zitakazojumuishwa katika maonyesho ya yst 2019 zitakuwa katika nyanja mbalimbali kuelekeza wanafunzi namna ya kufanya tafiti za kisayansi na ugunduzi wa teknolojia umefanikishwa na wadhamini wetu shell na karimjee Jivanjee Foundation" amesema kamugisha.

amesema Wanasayansi chipukizi watakaofanya ugunduzi mzuri mzaidi watazawadiwa pesa ,medali ,matengenezo ya maktaba ya shule pamoja na vitabu.

 Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Tasisi ya Tanzania Young Scientist(YST), Dr. Gozbert Kamugisha  akizungumza jambo na Waandishi wa habari
 Mkurugenzi wa Karimjee Foundation, Yusuf Karimjee akieleza Waandishi wa habari namna gani tasisi yake ilivyoweza kudhamini wanafunzi 27 tangu mashindano na maonyesho ya Sayansi yaanze nchini.
 Afisa uhusiano wa kampuni ya Shell Tanzania Patricia Mhondo akieleza malengo ya kampuni yake kwa kuwaendeleza vijana katika sekta ya Sayansi.

Sehemu ya Waandishi wa habari walioshiriki katika mkutano huo juu ya maonyesho ya Wana Sayansi Chipukizi kwa mwaka 2019

Post a Comment

Previous Post Next Post