UWEKEZAJI KATIKA TEKNOLOJIA ZA KISASA ZA UCHIMBAJI MADINI MIGODI YA TWIGA NA BARRICK WAPONGEZWA NA MAOFISA WA HAZINA

 

MAAFISA kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina wametembelea mgodi ya Twiga Minerals Corporation ya North Mara, uliopo wilayani Tarime na Bulyanhulu uliopo wilayani Msalala inayomilikiwa kwa ubia kati ya Kampuni ya uchimbaji ya Barrick na Serikali ya Tanzania ambapo uliweza kushuhudia operesheni mbalimbali za uchimbaji wa dhahabu kwa kutumia teknolojia za kisasa ikiwemo teknolojia ya uchimbaji wa dhahabu bila kulazimika kushuka chini ya ardhi kama inavyofanyika katika migodi mingine nchini.


Pia ujumbe wa maofisa hao ulitembelea miradi mbalimbali ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) hususani katika sekta za elimu,afya na maji katika maeneo yanayozunguka migodi hiyo ikiwemo mradi wa kilimo biashara  cha umwagiliaji uliopo Namongo wilayani Tarime unaolenga kuwezesha vijana wanaoishi katika vijiji viliyopo jirani na mgodi wa North Mara.


Ujumbe huo baada ya ziara hiyo ulipongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni ya Barrick na Twiga ambao kwa kiasi kikubwa umeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya uchimbaji madini nchini , kuchangia pato la taifa kupitia sekta hiyo na kufanikisha miradi ya kijamii ya kuboresha maisha ya wananchi hususani wanaoishi jirani na migodi.







Post a Comment

Previous Post Next Post