Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mheshimiwa Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, amewashukuru viongozi wa CCM, wanajumuiya na wananchi wa Kata ya Goba kwa mapokezi mazuri, mshikamano na upendo mkubwa wakati wa ziara yake ya kushukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.
Mheshimiwa Kairuki amewapongeza wananchi kwa umoja na kujitokeza kwa wingi, akiahidi kuendelea kusimamia maendeleo yao. Ameweka kipaumbele kwenye maji, barabara, elimu na afya, pamoja na kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu kupitia utoaji wa viti mwendo.
Amesisitiza kuwa ni kiongozi wa vitendo na kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na kuamini juhudi za maendeleo kwa ustawi wa Goba na Kibamba kwa ujumla.
#angellahkairuki
#kibambakwanza
#wizarayamawasilianonateknolojiayahabari
















