SERENGETI FIESTA YA
BAMBA JIJINI MWANZA
TAMASHA la muziki la Sertengeti fiesta linalodhaminiwa na
kinywaji mashuhuri cha Premium Serengeti limeanza kwa kishindo mwishoni mwa
wiki ambapo zaidi ya wakazi 30,000 walihudhuria na kusababisha msisimko mkubwa kwa
wasanii waliotumbuiza tamasha hilo kwenye Uwanja wa CCM kirumba Jijini Mwanza.
Tamasha la Mwanza, ambalo lilikuwa la aina yake, lililojaa
shangwe na msisimko mkubwa, lilitumbuizwa na wasanii kama Diamond Platinum,
Linah, Shilole, Ally Kiba, Mr. Blue, Young Killer, Ney wa Mitego, Madee, na
wengine wengi.
Onyesho la mwaka huu limevuta hisia za wengi hasa wataalam
wa burudani walioipongeza kampuni ya Serengeti Breweries kwa kuwa mfano mzuri
wa burudani bora.
Kampuni ya Serengeti imewahakikishia watanzania kwamba kwa
kipindi chote cha kiezi mitatu ya Serengeti fiesta watatoa burudani ya pekee na
isiyo na kifani.
Abaadhi ya mikoa ambako Serengeti itapita ni pamoja na Kahama, Bukoba, Musoma, Shinyanga,
Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma, Tanga,
Moshi, Arusha, Mtwara and Dar es salaam na hatimaye Jijini Dar es Salaam Oktoba
18 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo, meneja wa
bia ya Serengeti, Rodney Rugambo alisema kwamba uongozi wa kampuni ya Serengeti
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, kutokana na uzoefu kutoka kenywe
matamasha mbalimbali ya fiesta kwa miaka iliyopita, tamasha la mwaka huu
limekuja na muonekano mpya, vionjo vipya na burudani kabambe.
“kwa mwaka huu, watanzania wajiandae kupata burudani ya
kukata na shoka kutoka kwa wasanii maarufu, mashuhuri na wenye vipaji. Fiesta
si kunya peke yake, pia kushuhudia vipaji mbalimbali vya mziki kutoka kwa
wasanii mbalimbali wenye vionjo tofauti,” alisema Rugambo.
Amesema ia kwamba kwa kipindi hicho cha miezi mitatu,
burudani la fiesta litaambatana na mashindano ya mpira wa miguu yanayojulikana
kama Serenegti Soccer Bonanza.
Pia kutauwa na mashindano ya kucheza muziki… Serengeti Dance
la Fiesta na vilevile mashindano ya kuimba yatakayo jikita zaidi kwa wasichana
– Serengeti Supa Nyota Divas – ambapo mshindi katika kila mkoa atakwenda
kushindana na mshiriki kutoka Jijini Dar
es Salaam.
.jpg)


