Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi
Karrim (kushoto), wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), akitoa
maelezo ya ujenzi wa mradi wa daraja la kisasa la Kigamboni kwa Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick (wa tatu kulia), aliyefuatana na Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi kutembelea mradi huo, Dar es Salaam
jana. Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Ramadhani Madabida.
Pix No. 8
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick (wa pili
kushoto), akimsikiliza kwa makini Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (wa tatu kushoto), wakati huo huo,
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Ramadhani Madabida
(wa tatu kulia), akimsikiliza Mhandisi
Karrim Mataka wa NSSF (wa pili kulia), wakati Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
walipotembelea mradi wa daraja la Kigamboni, Dar es Salaam jana.
Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Mhandisi John Msemo (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick (wa pilia kulia) aliyefuatana na Wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), walifika kukagua maendeleo ya
mradi wa daraja la kisasa la Kigamboni, Dar es Salaam jana. Wa tatu kulia ni
Mwenyekiti wa CCM mkoa, Bw. Ramadhani Madabida.


