Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiwaeleza wajumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi kuhusu kuanza kutumika kwa sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015 na jinsi itakavyobadilisha baadhi ya mifumo ya kibiashara,wakati wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) Leo Jijini Dar es Salaa
Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi Bw.Nicholus Duhia akimshukuru Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade kwa kuhudhuria ufunguzi wa semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) na kuahidi kuwa washiriki wazuri katika mabadiliko katika sekta ya Kodi nchini,wakati wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) Leo Jijini Dar es Salaa
1-
Baadhi
ya wajumbe wa semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya
Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) wakimsikiliza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade
2-
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akimueleza jambo
Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi na mwenyekiti wa Kamati ya
sekta ya Umma Bw.Nicholus Duhia, katikati ni Bi. Diana Masalla Meneja Elimu kwa
Mlipakodi.
Na Hassan Silayo MAELEZO
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
imedhamiria kufikia malengo yake katika ukusanyaji wa kodi ili kuiwezesha
serikali kufikia shilingi trilioni 22.3 iliyojiwekea katika bajeti ya mwaka wa
fedha 2015/2016.
Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar es
Salaam na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade wakati wa
Semina ya wahasibu iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa
ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) ikiwa na lengo la kujadili kuhusu masuala ya
kodi, bajeti na uchumi kwa ujumla.
“Moja kati ya malengo tuliyojiwekea
sisi kama mamlaka ni kuisaidia serikali katika ukusanyaji wa mapato tukiwa na
lengo la kuiwezesha kufikia kiasi cha shilingi trilioni 22.3 zilizopangwa
kutumika katika mwaka huu wa fedha” Alisema Bw.Rished.
Akieleza kuhusu sheria mpya ya kodi iliyoanza
kutumika julai 1, 2015 Bw. Rished alisema kuwa kuwa sheria hii inategemewa
kubadilisha baadhi ya mifumo ya kibiashara nchini.
Pia alieleza kuwa kitu muhimu kwa
sasa ni wajumbe wa bodi hiyo kukaa na kuipitia sheria hiyo na kuangalia
mabadiliko yaliyomo na wao kama wadau katika sekta hiyo kusaidia katika
kuboresha mazingira ya kibiashara.
Naye Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya
wahasibu na wakaguzi Bw.Nicholus Duhia alimshukuru Kamishna Mkuu kuhudhuria
semina hiyo na kuahidi kuwa washiriki wazuri katika mabadiliko ya sekta ya Kodi
nchini
“Ndugu Kamishna Mkuu, umekuwa
ukishirikiana na kufanya kazi kwa karibu na bodi hii, hivyo tunakuahidi baada
ya kumaliza semina hii tutakuwa washiriki wazuri hasa katika mabadiliko ya sekta
ya Kodi nchini” Alisema Bw. Duhia.
Aidha, Mshiriki wa Mafunzo hayo na
muwakilishi kutoka Jubilee Insurance Bi. Hellena Mzena alisema kuwa kikubwa
anachotegemea kujifunza kutoka kwenye semina hiyo ni jinsi gani sekta ya Bima
ilivyoguswa kwa mara ya kwanza katika Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la
Thamani ya mwaka 2014 na jinsi gani wataenda sambamba na mabadiliko hayo.
1-
Bw. Yona Kilagane akiwasilisha mada wakati wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) Leo Jijini Dar es Salaa.
1-
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo.