Na Mwandishi Wetu
Makamu Mwenyekiti Taifa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Dominata Rwechungura amesema Watanzania hawataendelea kukubali kudanganywa na wanasiasa kwa kuwa mambo yanayofanywa na serikali iliyopo madarakani yapo dhahiri.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es
Salaam jana, Rwechungura alisema wameamua kutuma ujumbe kwa Watanzania wote
kuwa wakatae kudandanganywa na wachambue maneno wanayoelezwa na wanasiasa
wasioitaka mema nchi.
“Tunaongea na Watanzania wote, wafanyakazi, wakulima na hata
watoto wa shule za awali maana TLP chama chetu kinagusa maslahi ya nchi, kuna
baadhi ya wagombea urais wamechukua fomu wamejinadi na kuteuliwa tunashitushwa
na kauli zao,” alisema Rwechungura na kuongeza:
“Kauli zao zinatupa ukakasi kama Watanzania kauli zao zina
mashaka, zinaonyesha kuvunja amani ya taifa, zinaonyesha kutugawa, si za kweli.
Mfano mtu unasema endapo sitashinda sitakubali kumuachia Mungu maana yake
utafanya vurugu nchi haitatawalika watu watapigwa, watasambaratika,
wafanyabiashara watapoteza vitu, utavunja amani ya nchi watu hawataenda
msikitini wala kanisani.”
Alibainisha, TLP wanaye mgombea urais na wao ndio wa kwanza
kufanya mkutano mkuu, Mei 9, 2020: “Tulijiridhisha kazi zote zilizofanywa na
Rais Dk. John Magufuli, tukaangalia na ilani yetu ya uchaguzi uliopita,
tuliahidi kusomesha wanafunzi bure, tutajega hospitali tutajenga barabara,
tukasema tukichukua serikali tutahamia Dodoma ili kupunguza matumizi yafedha za
walipa kodi.
“Yale yote tuliyoainisha kwenye ilani yametekelezwa na Mtanzania
mwenzetu, ndugu yetu Dk. Magufuli tofauti yetu ni itikadi ya chama kila mmoja
ana katiba yake, yeye ana CCM yake mimi nina TLP yangu.”
Alisema, Tanzania imepata mtu mchapakazi, msema kweli anayeletea
maendeleo je wamkatae? Kila alichokifanya kinatumiwa na wapinzani na wana CCM,
sasa wanamchukia kwa sababu gani: “Watu wanakwambia aliyekupenda mpende,
Dk.Magufuli ametupenda sote,” alisema na kubainisha:
“Sisi mgombea wetu nawatangazia leo (jana) ni Dk. John Magufuli
mzaliwa wa Chato, Mtanzania mwenzetu, tutampata wapi rais wa Watanzania
atakayesimama katika kipindi cha majanga kama Corona, nchi nyingine wamekufa
wengi lakini Rais Magufuliamesimama na sisi awaokoe Watanzania wake akatutaka
tuombe kwa Mungu kwa siku tatu.
“Hatuwezi kukubali kuona Rais Magufuli akipakwa matope,
tunawaomba wagombea urasi wanapotoa taarifa zao wafanye utafiti kila kitu kipo
wazi kwenye tovuti za taasisi za umma, kwa kuwa Watanzani wa sasa si wa zamani
wanajua huyu amesema uongo huyu amesema kweli.
“Usikurupuke kutoa data za uongo, mtu ana chuki zake
anazichanganya na siasa unamuona hadi sura imembadilika kwa chuki zake, kataeni
tumesituka TLP tumeanza kuwapima wote tumechukua kauli zao tunaona mbona kauli
hii si ya uzalendo mbiona inatuletea shida, jinadi sema hoja zako jenga hoja
kwa hoja watananzania wakuelewe.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vijana Taifa TLP Ivan Maganza,
alisema chama hicho kimeamua kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuwa vijana wanao
wajibu kueleza umma namna mambo ambayo serikali imewafanyia na
kuomba Rais Magufuli awe rais kwa awamu nyingine ya miaka mitano.
“Vijana tulikuwa na changamnoto ya ajira kwa kujenga viwanda
ambapo huo unakuwa muarubaini wa tatizo la ajira, amefungua mradi wa kuzalisha
umeme ambapo utapunguza gharama za umeme na kumuondolea adha mwananchi kwa
kulipa gharama kubwa ya umeme na wawekezaji wataongezeka,” alisema Maganza.