Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MKUU wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo
kigamboni,Profesa , Shadrack Mwakalila
ameagiza wanafunzi wa chuo hicho waliojiunga katika mwaka wa Masomo wa
2017 kutojiusiha na masuala ya siasa pindi wanapokuwa chuo na badala yake
wazingatie katika suala zima la taaluma hili waweze kupata kile kilicho
wapeleka chuoni hapo.
Profesa Mwakalila amesema hayo alipokuwa akizungumza na
wanafunzi wa Mwaka wa kwanza juu ya nini wanatakiwa kufanya wakiwa chuoni hapo
na kutambua nini cha msingi kilichowaleta.
"Hapa sio mahali pakufanya Siasa ni sehemu mliyokuja
kuchua taaluma kamwe msikubali wanasiasa kuwatumia kwa ajili ya maslahi yao
kwani mkifanya hivyo mtakuwa mmepoteza lengo ambalo limewaleta hapa katika
kufanikisha malengo yenu ya kitaaluma"amesema Profesa Mwakalila.
Profesa Mwakalila ameongeza kuwa kama wanavyojua chuo hicho
kimetokana na Mhasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius .K. Nyerere hivyo wanapaswa
kufuata maadili na kuwa waadilifu hili kuweza kumuenzi mhasisi wa Taifa ambaye
alikuwa na ndoto ya kuwa sehemu hiyo iweze kupika viongozi wenye maadili mema
kwa Taifa hili.
alimaliza kwa kutoa wito kwa wote waweze kukazana katika
masomo yao hili waweze kuwa alama ya chuo hicho pindi wanapomaliza masomo yao
na kufika hapo kwao isiwe majuto.
Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akikazi jambo juu ya kuwa na maadili shuleni
Sehemu ya Wanafunzi wa wapya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni wakifatilia hotuba ya Mkuu wa chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila