Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii
Rais Mstafu
wa Awamu ya tatu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete(MB)
Wameongoza Maelfu ya Watanzania katika kuaga Mwili wa aliyekuwa Mtangazaji wa
kituo cha Clouds Fm Marehemu Ephrahim Kibonde nyumbani kwa Baba yake Mbezi
Beach Jijini Dar es Salaam.
Katika ibada
hiyo ya kuto aheshima za mwisho viongozi wengine wa kiserikali waliohudhuria ni
pamoja na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo , Dr Harrison Mwakyemb,
Waziri wa Madini Doto Biteko,Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William
Lukuvi ,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda , Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Daniel Chongolo.
Viongozi
wengine waliofika katika Msiba huo ni pamoja na Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti
wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Suleiman
Jaffo, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
Aidha waandishi
wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini kwa umoja wao waliweza kufika katika
msiba huo na kutoa faraja kwa wafiwa ambapo safari ya kuelekea Makaburi ya
kinondoni kumpumzisha mpendwa wetu
Ephrahim Kibonde.
Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete(MB) akisaini kitabu cha Maombolezo wa Ephrahim Kibonde nyumbani kwa Baba yake Mbezi Beacha Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstafu wa Awamu ya tatu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete(MB), Wakizungumza na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga mara baada ya kusaini kitabu cha Maombolezo.
Rais Mstafu wa Awamu ya tatu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete,akiteta na Baba yake Ephrahim Kibonde kabla ya kuaga Mwili wa Mrehemu nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara akitoa pole kwa Dada wa Marehemu Sara Kibonde wakati wa zoezi la kuaga mwili wa Marehemu Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiteta jmabo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makzi mara baada yakuaga Mwili wa Marehemu Ephrahim Kibonde.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondomni Daniel Chongolo akibadilishana mawazo na Wadau wa habari waliofika katika Msiba wa Ephrahim Kibonde
Mmoja wa Waombolezaji wakifika Msibani huku wakiwa wanasaidiwa na wanandugu wengine