Na. Chollomaster
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Daniel Chongolo amemtaka mkandarasi wa kampuni ya NAMIS CORPORATE LTD ambaye anajenga soko hilo kuongeza kasi ya ujenzi huo ili wafanyabiashara waweze kurudi kwenye eneo lao .
Mhe. Chongolo amesema hayo alipofanya ziara katika Soko la Tandale na kuwakuta wafanyabiashara Katika mazingira yasiyorafiki hali inayopelekea usumbufu wa shughuli zao na kumuelekeza mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ujenzi huo ili kuwondokana na adha inayowakabili.
Amesema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha miundombinu yote ya Masoko ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara na kuendesha maisha yao na hivyo kuwezesha halmashauri kufikia malengo .
Amefafanua kuwa mradi huo wa Soko la kisasa unajengwa kwa gharama ya sh.Billion 8.7 fedha ambazo zimetolewa na Serikali kuu na kwamba tayari Mkandarasi huyo ameshalipwa fedha zote na hivyo kusisitiza kwamba anapaswa kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi yake kwa wakati.
Awali meneja kutoka Kampuni hiyo iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa Soko hilo Mkandarasi James Msumari alimueleza DC Chongolo kuwa ujenzi huo utachukua miezi 12 Jambo ambalo alionesha kutoridhishwa na Muda huo na kusema kuwa hakuna sababu ya kutumia muda mrefu kwa kuwa fedha wanazo hivyo wanapaswa kukamilisha ujenzi kwa makubaliano yaliyoingiwa.
Kwa upande wa
Mhandisi Msumari amesema wamepokea maagizo na wako tayari kuyatekeleza ili waweze kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa eneo hilo.