Na Mwandishiwetu
Mgombea Urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Tundu Lissu amelazimika kubadilisha gari na kuanza kutumia gari ya Katibu Mkuu wa Chama Hicho John Mnyika kukwepa hoja kuwa amezunguka mikoa yote ya kanda ya ziwa na Kaskazini kwa kutumia gari ndogo huku akipita juu ya Barabara za Rami.
Lissu ambaye alikuwa akibeza maendeleo ya vitu kuwa ayana faida nchini lakini yeye amekuwa mtu wa kwanza kufaidi maenedeleo ya vitu kwa kutembea kwa rami kuanzia Dar es Salaam mpaka mikoa yote aliyopita kuomba udhamini.
Ubora wa barabara na Miundombinu yetu ndio umesababisha yeye leo kutumia muda mchache kuzunguka mikoa ya kati, kanda ya ziwa, Kaskazini na sasa yupo nyanda za juu kusini akitafuta wadhamini.
Lissu amekuwa kipofu kabisa kwa kushindwa kuona kuwa amewezaje kutembea na Corola katika mikoa yote hiyo kwa kipindi cha muda mfupi huku akiomba wadhamini jambo ambalo miaka ya nyuma walifanya kazi hiyo kwa kutumia Helkopta.
Aibu ya Lissu imemkuta tena mkoani Mbeya ambapo aliwasili jana usiku na kulazimisha maandamano ya usiku na kujikuta yuko peke yake bila ya kubugudhiwa na mtu kwani lengo la Maandamano hayo ilikuwa ni kutafuta chochoko kwa jeshi la Polisi lakini Polisi kwa weledi mkubwa wakamuacha aendelee mpaka alivyojiona mjinga na kuamua kwenda kulala.
Jambo hili la kutoka bugudhiwa na Polisi limemkera na kuzidi kuongezea wazimu Lissu ambaye amefika mkoani mbeya na kushindwa kuomba wadhamini katika hatua ya kugombea urais na kujikuta akimshambulia Naibu Spika Dk Tulia Akson jambo ambalo limeacha maswali mengi kwa wana mbeya kwa kuona kuwa kweli mgombea huyu ana matatizo kichwani mwake.
Uzwazwa huu Lissu ajaunza mbeya kwani katika mikoa yote ambayo amepita amejikuta akionesha makovu yake na na kujitapa kuwa yeye ni gwiji wa sheria lakini ameshindwa kusimamia sheria kwa kuanza kuvunja kwani anafanya kampeni kabla ya wakati.