Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema kwa kushirikiana na Viongozi wenzake wa wilaya hiyo tayari wameanza mchakato ambao unalenga kumaliza kabisa tatizo la ukosefu wa madawati kwenye shule zote Wilayani humo hadi kufikia September 30, 2020.
•
"Tuna upungufu wa madawati 2699 (msingi na sekondari) na tumeanza kutengeneza madawati, ikifika September 30 tatizo hili litakuwa limeisha Kisarawe, na tutatengeneza kwenye karakana yetu wenyewe hapa Kisarawe"-DC Jokate
•
DC Jokate amesema Wilaya hiyo kwa sasa inaongeza shule mpya mbili, Kisarawe Secondary ambayo itajengwa Kazimzumbwi na Homboza Primary School>>"nampongeza sana Waziri Jafo kwa uwekezaji mkubwa alioufanya kwenye elimu"