Muite "ISAAC LUGONZO MALIYAMUNGU" fagio la chuma lililosafisha kila aina ya uchafu usiompendeza Binamu yake IDD AMIN DADA. Alivunja ghala la silaha Lubiri, Kampala na kuiba silaha zote na baadae akawaongoza wanajeshi waasi na kuipindua serikali ya Obotte...
:
Maliyamungu alikuwa ni mtu wa kabila la Kakwa ambalo ndilo lilikuwa kabila la Idd Amin Dada, alizaliwa Nchini DRC Congo wakati huo ikiwa inaitwa Zaire na haijulikani alizaliwa mwakagani haswa. Aliondoka Nyumbani kwao Zaire na kuingia Nchini Uganda kutafuta kazi ambapo alifanikiwa
:
Maliyamungu alipata kazi ya Ulinzi katika kiwanda cha Nyanza huko mjini Jinja. Wakati akiendelea na kazi mnamo mwaka 1967 alifanikiwa kupata nafasi na kuingia jeshini kwa msaada mkubwa wa Binamu yake Idd Amin ambaye kwa wakati huo alikuwa makamu mkuu wa jeshi la Uganda.
:
Inasemekana kuingizwa jeshini kwa Maliyamungu ulikuwa ni muendelezo wa agenda za siri za Idd Amini kuajiri vijana wa kabila lake la Kakwa ili kuandaa mazingira mazuri ya kufanya mapinduzi baadae. Mnamo mwaka 1970 Idd Amin alimpandisha Maliyamungu cheo na kuwa coplo ambapo alihamishiwa kwenye vikosi vya Anga vya mjini Entebbe,
:
Akiwa huko Entebbe Maliyamungu aliendeleza mpango dhalimu wa kuwaingiza vijana wa kabila la kakwa kutoka nchini Zaire na Sudani ili kutekeleza adhma yao ya kuipindua nchi ya Uganda iliyokuwa chini ya madaraka ya Milton Obotte kwa wakati huo...
#Maliyamungu
#Partone sehemu ya pili kesho🏃
Stori tamu hii Najua kuna watu watasema #SioSawa niendelee