KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA MBULU-MANYARA, YAMALIZA MGOGORO KATIKA KIJIJI CHA DAMANGA,KATA YA HASHKESH (JIMBO LA MBULU VIJIJINI.




Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Komred Kheri James,ameiongoza kamati hiyo mapema Leo kufika katika Kijiji cha Domanga,ambacho hivi karibuni yalitokea Mapigano baina yao na Kusababisha Kujeruhiwa Vibaya Kwa Wananchi Wawili.                                     


Wakizungumza katika Mkutano huo,Wananchi wamebainisha kuwa chanzo cha Mgogoro ni kuhisi kuwa zoezi la kudhibiti maeneo yaliozuiwa kwa malisho katika Kijiji halisimamiwi kwa Haki na Usawa.                                 

Akiwa ktk mkutano huo Komred Kheri James aliagiza kufunguliwa kwa Ofisi ya Kijiji iliokuwa imefungwa na kuzungushiwa Miba na Wananchi wenye Hasira Kali,na kisha aliwasikiliza wananchi wote wa Jamii ya Wahadzabe na Wadatogwa,na kuwaeleza umuhimu wa kutumia Vikao Vyao vya Kijiji kujadili na Kuamua Mambo yao.


Lakini pia Komred Kheri James aliwaeleza Madhara ya matumizi ya nguvu na uharibifu wa Mali,kuwa Vitendo hivyo havikubaliki na nikinyume cha sheria.Kamati ya Usalama imezipatanisha pande zote Mbili,na imesistiza matumizi ya Vikao vya Kisheria kama njia ya kujadili na kuamua mambo yote yanayo husu kijiji na wananchi.                                    


Kamati ya usalama ilikamilisha ziara yake kwa kuwatembelea wananchi wawili waliojeruhiwa katika Mapambano hayo,hali za majeruhi sasa zimeanza kuimarika,na hali ya usalama katika kijiji cha Domanga imerejea na wananchi wameanza kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.          


Ziara hii pia ilihudhuriwa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini pamoja na Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Heshkesh ambao walisaidia sana mazungumzo na hatimae muafaka kwa wananchi wote wa Domanga.                                
#Kwapamoja,tuna
ijenga Mbulu yetu..

1 Comments

Previous Post Next Post