Na lilian Ekonga......
Chemba ya biashara kimtaifa ya Dubai imesaini hati ya makubaliano ( MoU ) na Chemba ya biashara ,Viwanda, Kilimo Tanzania (TCCIA) ili kuimarisha Ushirikiano na kukuza biashara na uwekezaji baina ya pande mbili utakaohusisha Ujuzi,kubadilishana taarifa,kuchunguza fursa za kibishara na uwekezaji.
Makubaliano hayo yalitiwa saini leo jijini Dar es salaam na Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chambers Mohammad Ali Rashed Lootah na Mwenyekiti wa Bodi ya TCCIA, Vicent Bruno Minja katika Kongamano la Biashara “Kufanya Biashara na Tanzania” lililoandaliwa na Dubai International Chamber kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali, ikiwemo Ubalozi wa UAE na Tanzania, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
Akizungumza katika kongamano hilo Waziri wa Viwanda na Biashara Suleiman Jafo amesema makampuni ya Kitanzania yapaswa kuchangamkia fursa zilizopo Dubai, ikiwemo sekta ya Nishati na madini, Dawa na vifaa tiba, Kilimo, Uzalishaji viwandani na uendelezaji wa miundombinu na teknolojia ili kusaidia kukuza Uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Rais na Mtendaji Mkuu wa Chemba ya Dubai Mohammed Ali Rashed Looth amesema misheni hiyo ni sehemi ya ahadi yao ya dhati ya kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kibiashara Masoko yenye fursa barani Afrika .
" Misheni hii inatoa fursa ya kipekee ya kujenga madaraja ya Ushirikiano kati ya Jumuiya za biashara za Dubai na Tanzania kufungua njia mpya za ushirikiano wa kiamkakati zitakazochangia ukuaji wa pande mbili na ustawi" amesema Mohammed
Naye rais wa TCCIA Vicent Minja amesema Makubaliano hayo yatasaidia thamani ya Biashara na Uwekezaji Kukuwa kwa kasi Tanzania
Amebainisha kuwa thamani ya biashara isiyohusisha mafuta kati ya Tanzania na Dubai ilikua kwa 9% mwaka 2023, ikifikia Dola za Kimarekani bilioni 2.7. hadi kufikia mwisho wa Septemba 2024, jumla ya makampuni 274 kutoka Tanzania yamesajiliwa kama wanachama wa Dubai Chamber of Commerce.