WANAFUNZI 80,000 SHULE ZA MSINGI WAPATA ELIMU YA USALAMA BARABARANI


Na Mwandishi Wetu
Jumla ya Wanafunzi 80,000 kutoka katika Mikoa ya Dar es Salaam, Ruvuma, Arusha, Kilimanjaro, Geita na Ruvuma wamenufaika na mafunzo yatolewayo na Kampuni ya Puma kuhusu usalama Barabarani.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usalama Barabarani kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania Bara na Visiwani,uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Naibu Waziri Masauni alisema tangu program hii ianzishwe jumla ya wanafunzi 80,000 wamenufaika lengo ikiwa ni kuwalinda watoto hawa ambao ni Taifa la kesho na madhara yanayotokea barabarani ikiwemo ajali.
“Sote tunagundua maendeleo ya Taifa lolote yanaletwa na watu, watoto hawa ni Taifa la kesho tunaotegemea watatuletea maendeleo,Serikali tunafanya juhudi za makusudi kuwalinda watoto hawa na tayari takribani watoto 80,000 washanufaika na mafunzo haya na lengo letu tuwafikie wengi zaidi” alisema Masauni
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma, Dominic Dhanah alisema wao kama kampni ya mafuta na wadau wakubwa wa usalama barabarani watajitahidi kuzifikia shule nyingi zaidi na kuisaidia serikali kulinda viongozi hao ambao anaamini ni nguvu kazi ya Taifa hapo baadae.
“Sisi Puma tukishirikiana na Kikosi cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi na wadau wengine tutaendelea kuhakikisha tunalinda maisha ya wanafunzi hawa na mpango wetu ni kuzifikia shule nyingi zaidi katika mpango huu wa kutoa elimu kwa wanafunzi” alisema Dominic

 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Usalama Barabarani kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania Bara na Visiwani ambao  utahusisha shule 95.Uzinduzi huo umefanyika leo Makao Makuu ya Kampuni ya Puma, jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma, Dominic Dhanahambao ni wadhamini wakuu wa Mpango wa Usalama Barabarani kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania Bara na Visiwani, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango  huo uliofanyika  leo Makao  Makuu ya Kampuni hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya AMEND inayoratibu Mpango wa Usalama Barabarani kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania Bara na Visiwani,Tom Bishop akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliozinduliwa leo na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani).Uzinduzi huo umefanyika leo Makao Makuu ya Puma,jijini Dar es Salaam

Post a Comment

Previous Post Next Post