Na Humphrey Shao
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako amewataka Vijana wa kitanzania waliopata nafasi ya kusoma nchini Uchina wazingatie maadili huili wasije wakalitia aibu Taifa uko ugenini
Waziri Ndalichako amesema hayo mapema leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza katika hafla maalum ya kuwaga vijana waliopata Ufadhili wa masomo kwenda kusoma Uchina ambao wameagwa leo nchini katika ofisi za ubalozi wa china
"Niwatakie tu masomo mema lakini mnachotakiwa ni kuzingatia maadili na kuachana na mamboa mabyo yapo kinyume na utaratibu wa nchi ya wenzetu niliambiwa kuna baadhi yenu mkifika huko mnaacha masomo na kuanza kuwa wafanyabiashara na waambia nyie ni sehemu tu ya watu waliopata nafasi kutoka Tanzania hivyo mjue kuna watu Milioni 55 wapo nyuma yenu" Amesema Ndalichako.
kwa upande wake Balozi wa China Nchini Tanzania , Wang Ke amesema serikali yake imeongoza idadi ya wanafunzi zaidi kutoka Tanzania tofauti na Mwaka jana mara baada ya rais wa nchini hiyo kuagiza vijana wangi wa kiafrika wakapate nafasi ya kusoma nchini humo.
ametaja kuwa serikali yake ipo bega kwa bega n nchini ya Tanzania kuhakikisha inasaidia katika upatikanaji wa wataalamu mbalimbali ambao watakuja kusaidia Tanzania katika kipindi hiki cha mapinduzi ya Viwanda.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akitoa nasaha kwa Vijana wa kitanzania waliopata nafasi ya kwenda kusoma china wakti wa hafala fupi iliyofanyika katika ubalozi wa China nchini Tanzania
Mmoja ya Wanafunzi waliopata ufadhili wa kusoma china akisalimiana na Balozi wa China na Waziri wa Elimu, Prof Joyce Ndalichako