HU NI UONGO ULIOPITILIZA...!!! TUNDU LISU ACHA KUONGOPEA WANANCHI


Na Macdeo Mackeja Shilinde

Tuwekane sawa kidogo kuhusu mambo ya uongo ambayo ameongea ndugu TUNDU LISU mgombea uraisi kwa nafasi kupitia chama Cha demokrasia na maendeleo.

HIFADHI YA TAIFA YA BURIGI
Mwanzo kabisa hi hifadhi ya taifa ya burigi kabla kupandisha hadhi kuwa hifadhi ya taifa ya wanyama pori, Lili kuwa ni pori moja wapo ya mapori ya hifadhi ya serekali ambalo linapatikana mkoa wa Geita,Hili pori lilianzishwa mwaka 1980 Kama pori la hifadhi la akiba.
Katika ukanda huo kwa maana ya mikoa ya Geita na Kagera yalikuwa yanapatikana mapori Kama vile:-
Burigi
Kimisi
Biaramulo
Kibanda na
Rumanyika.

Mwaka 2018-2019 kwenye bunge la bajeti,wizara ya utali walipeleka hoja bungeni ya kuomba kupandishwa hadhi baadhi ya mapori ya akiba na kuwa hifadhi za taifa,mapori hayo ni Burigi,Biaramulo,kibanda na rumanyika.
Haya mapori yote yapo katika ukanda muhimu Sana wa ki ikorojia.
Lengo la wizara ya utali kupeleka hiyo hoja ni kwa sababu ya kupanua utali na kuongeza mapato ya taifa ndani ya miaka Saba ili yafikie bill.16 USD yani maana yake wastani wa watali kufikia mil.8 kwa miaka hiyo Saba.
Wa bunge wote wa bunge la Tanzania walipitisha na wakiwemo na wabunge wa Chadema na yule mtoa vimemo vya uongo kwa mgombea wao bwana Mnyika alikuwepo kwenye kupitisha maamuzi hayo.

Lakini wabunge walikubaliana hayo kwa hoja nyingine ya msingi.
Biaramulo,Burigi na kimisi haya yote yaliunganishwa na kuwa hifadhi ya taifa kwa jina la BURIGI na mapori haya yote yamezungukwa na kata 18 na vijiji 48.

UWANJA WA NDEGE WA CHATA
Kutokana na kupandishwa hadhi mapori hayo na kuwa hifadhi ya taifa kwa namna moja au nyingine ni lazima kuwepo kwa uwanja wa ndege ili uraisishe utali na kupanua wigo wa utali.
Sasa ndio unaona uongo wa huyu mgombea wa Chadema bwana TUNDU LISU kwamba uwanja wa ndege raisi MAGUFULI kajenga kwa ajiri yake.

RAI YANGU KWA WATANZANIA
Tumpinge vikali Sana huyu muongo wa taifa na mchonganishi wa taifa letu kwa hu upotoshaji anaoufanya kipindi Cha kuelekea kwenye kampeni za uchaguzi mkuu.

Post a Comment

Previous Post Next Post