Na Mwandishi Wetu, Dar.
Nilipofanya field katika gazeti la Tanzania Daima baada ya kumaliza diploma yangu wakati ule wakiwa pale klabuni Billcanas nilipata kumuuliza mhariri mmoja juu ya falsafa ya gazeti hilo:
1. Kama ni ni la upinzani na kwamba linatekeleza falsafa ya mrengo huo na kutetea kila kitu cha mrengo huo kiwe kibaya au kizuri? Akajibu ni kitu flani kama hicho lakini sio kiviile;
2. Nikamuuliza ni la kitaifa? Kwamba linapigania itikadi ya Tanzania na agenda ya mageuzi katika nchi? Akaguna tu mmmh dogo hapa ukileta hizo unaondoka!
Hii ndiyo siku niliacha kuamini gazeti la Tanzania Daima na nikamaliza field yangu nikafanyakazi kidogo na kusepa.
Leo nikacheka sana kumsikia Msemaji wa Chadema anahoji masuala kadhaa kuhusu kufungiwa kwa gazeti hilo.
Anasema sababu ni zipi? Kwangu sijaona barua waliyoandikiwa Daima wenyewe lakini sababu ya kwanza kubwa huhitaji kuona sababu zilizotunika na Serikali kuona hili gazeti halieleweki itikadi yake ni ipi kwa Taifa la Tanzania. Yani unagazeti anaongea kiongozi wa nchi kuhusu maendeleo haliandiki, akiongea mzungu kuponda maendeleo ya Tanzania lenyewe ndio habari kubwa front page!!! Mimi kuna wakati nilianza kuamini hawa Daima labda kuna viongozi wamewapa limbwata hadi huko nyuma wakawa hawagusiki!
Huku sio kukosoa bali ni uzandiki na unafiki wa kiwango cha usaliti kwa nchi. Yani gazeti unaliona nchi ikitukanwa ndio linashabikia halina stori nyingine za maana.
Kwa hiyo ndugu yangu Makene wala huhitaji kuomba copy ya barua kutoka kwa Mwenyekiti wako ambaye pia ndio mmiliki wa gazeti kuona sababu; sababu iko wazi gazeti hili lilishindwa kuwa na itikadi ya kitaifa kuanzia mwanzo hasa nini linataka kuachieve. Kagazeti yako mengi yanayokosoa au kufanya habari za uchunguzi kama Raia Tanzania na Jamhuri, mbona yanachapa kazi?
Angalia gazeti la Uhuru pamoja na kuwa ni la CCM, asilimia zaidi ya 90 linafocus kwenye Ilani na itikadi za chama hicho ambacho gazeti linaamini katika itikadi zake. Uhuru huwezi kukuta kila siku wanamwandamanau kumtukana Mbowe, Lissu au Zitto Kabwe na kuchapisha habari za uongo dhidi ya vyama vya upinzani na viongozi wake. Tanzania Daima lilikosa mwelekeo likajikuta linachanganya mambo.
Leo pia Makene anahoji gazeti limetuhumiwa na kufungiwa na Serikali hiyo hiyo aah sasa hapa napo Chadema wasinifanye nikahoji weledi wao katika utawala na nawaachia manguli wa sheria na taratibu.
Nafahamu Kuna vyombo vinapewa haki kuamua masuala fulani fulani kijamii sio kila suala liende mahakamani tu. Ndio maana wao wenyewe Chadema juzi wametimua wabunge wao kadhaa ni chama kimelalamika, kikaendesha kesi hakikuwaita kujitetea kikatoa hukumu! Nadhani wangeanza kujitathmini wao katika hili la mchakato wanalohoji!
Najua sio Chadema ni wengi watatoa matamko; MISA Tan wamegusa kidogo, Editors Forum ndio kwanza bosi wao mmoja kaonekana anashauriana na mabalozi flani wa nje kwanza na wengine wengi.
Lakini swali la kujiuliza ni Je, sote sisi tuliwasaidia Tanzania Daima kuwa na itikadi yenye kubaki kwenye misingi ya taaluma ya habari? Nimewaona mara nyingi wakiomba radhi kwa kukosea habari hii na ile hakuna aliyewasaidia kiitikadi wasimame na waenende vipi?
Lakini sio itikadi tu wakati pia taasisi moja ya habari anakofanyakazi rafiki yangu wa karibu kwa sasa ikiwa inahariri tamko walilotumiwa na taasisi moja ya nje walitoe, tufahamu tu kuwa hali ya wafanyakazi wa Tanzania Daima pamoja na kazi hiyo "kubwa" bado ni mbaya.
Waandishi wake wanamiezi kama sio miaka ya kukosa haki zao na kuishi kwa vijiposho. Hawa ni miongoni mwa waandishi wanaoishi kwa mizinga na kuungaunga makala na stori za ndani wapate mshiko.
Nawakumbussha wanaojifanya leo wanawatetea waache kusubiri umeme ukatike waishie tu kusema ayaaaaaaaaaa! Haisaidii.
*Mwandishi amepata kufanyakazi katika gazeti la Tanzania Daima*