- Emily anasema alipoanza kukimbia mtaani (Jogging) alikutana na kigingi cha watu kumkimbia kila alipokuwa anawasogelea.
- Anafafanua kuwa kulikuwa na watu wengi wanaokimbia, lakini ni yeye aliyekuwa akipata wakati mgumu katika kukumbia huko.
"Nimezoea maisha ya kubaguliwa kutokana na rangi yangu, niko huku Ujerumani mwaka wa tano sasa, so hata nilivyokuwa nikikatiza mtaani kwa ajili ya Jogging watu walinikwepa na wengine waliziba pua zao.
"Huwa inaumiza sana, lakini nashukuru kuona mtoto wangu hakutani na ninachokutana nacho mimi mwenyewe. Wakimtazama mtoto huwa wanamuona kama mwenzao, hivyo yeye yuko salama zaidi na wengi wanampenda kutokana na uchangamfu wake dhidi ya watoto wenzie" alisema Emily.
- Emily alisema alifurahi kusikia taarifa ya kuanza mazoezi ya kuchanganyika pamoja, kabla ya hapo walikuwa wakifanya mazoezi ya watu watatu watatu kiwanjani.
- Alisema hii nayo ilikuwa na changamoto zake. Alieleza kuwa walikuwa wanakwenda mazoezini wakiwa katika vazi la tahadhari na walikuwa wakivaa Mask (Barakoa) za kujikinga.
"Nilikuwa nimeshapona majeraha yangu, lakini nikawa namalizia program nilizokuwa nimepewa, lakini baadae nilifurahi kusikia tumepewa taarifa ya kuanza mazoezi ya pamoja tofauti na awali watu kuanza mazoezi ya kucheza watu watatu watatu kiwanjani.
"Mazoezi yale nayo yalikuwa na changamoto zake. Kufanya mazoezi huku umevaa Mask puani sio mchezo maana unashindwa kupumua vizuri, lakini ni utaratibu uliowekwa huwezi kuupinga ukaja na utaratibu wako" alisema.
- Mchapo unaofuata Emily atatuambia jinsi wachezaji wenzake walivyokuwa wakimchukulia baada ya kuambiwa waanze mazoezi ya pamoja, huku wakumuona wao kama tatizo kutokana na ugonjwa wa Corona.