MIRADI YA MAJI 354 IMEPOKEA FEDHA KUTOKA KWENYE MFUKO NWF, KUNUFAISHA WATU ML.5.3






MFUKO wa Taifa wa Maji (NWF) umesema, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2024, miradi ya maji 354 kati ya miradi 998 iliyopokea fedha kutoka mfuko huo imekamilika na kunufaisha wananchi wapatao milioni 5.3.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF),Wakili Haji Nandule amebainisha hayo leo Oktoba 31,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi kati ya wahariri na waandishi wa vyombo vya habari nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).


Amesema Hii ni kazi kubwa, na tutahakikisha fedha zinazokuja kwenye taasisi yetu tunaendelea kuzitoa na kuzielekeza maeneo husika ili wananchi waweze kupata huduma bora za maji.

"Hii ni taasisi ya fedha yenye lengo la kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya usambazaji majisafi kwenye maeneo yenye uhaba na utunzaji wa vyanzo vya maji nchini."

"Kwa hiyo,kubwa ni kukamilika kwa miradi 354 katika kipindi hicho na hadi kufikia Julai 2024, jumla ya shilingi bilioni 5.3 zimetolewa kama mikopo kwa mamlaka za maji,"amesisitiza Wakili Nandule.

Wakili Nandule ameongeza miradi hiyo inajumuisha uhifadhi wa vyanzo vya maji zaidi ya 92 ikiwemo chemichemi, vidakio vya maji, maziwa,Afisa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri akiongoza kikao hicho.


Aidha amesema wapokeaji wa fedha za miradi ya mfuko ni Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), mamlaka za maji na bodi za maji za mabonde.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mfuko wa Taifa wa Maji, Abadallah Mkufunzi Amesema katika kipindi cha Miezi 6 tangia wameanza kutoa mikopo tumekutana na changamoto mbalimbali ambazo zinabidi tuboreshe kanuni walizokuwa nazo

"Tumepokea na tutawapatia waatalaamu wetu tuoneka kama wataweza kuweza kwenye maboresho yetu ya kanuni zetu" amesema Mkufunzi.

Nae Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahiriri Tanzania, Deodatus Balile ameushauri mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) kujitanga mara kwa mara kwa kuzungumza waandishi wa habari ili jamii iweze kuwatambua.

"Niwaombe mjitangaze kwenye vyombo vya habari na ili muweze kujitangaza na wananchi waweze kufahamu na miradi yenu" amesema balile

Huduma zinazotolewa na mfuko zinatokana na majukumu yaliyoainishwa kwenye Sheria katika Kifungu cha 56 ((a) – (g)) kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kusaidia uwekezaji kwenye miradi ya maji na utunzaji wa vyanzo vya maji.

Post a Comment

Previous Post Next Post