Na Lilian Ekonga, Dar
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesema Zoezi la kubadilisha Noti ya zamani litaanza Rasmi tarehe 6 januari 2025 kwa kipindi cha miezi miatatu mpaka tarehe 5 aprili 2025, huku noti hizo zitafika ukomo na kutokuwa halali kwa malipo nchini na Duniani Kote.
Alikalika (BOT)imesema zoezi la kuondoa kwenye mzunguko Noti hizo za zamani za shilingi ishirini (20), mia (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000) na elfu kumi (10000) kwa matoleo ya mwaka 1985 hadi mwaka 2003, na noti ya shlingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010 zenye sifa zilizoainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.
Akizungumza na Waandishi habari leo octaba 31, Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Sarafu BOT Ilulu Ilulu amesema zoezi la ubadilishwaji litafanyika kupitia ofisi zote za benki na matawi yake nchini na kupitia benki zote za biashara.
"Baada ya tarehe hiyo mtu yoyote au taasisi yoyote inayomiliki fedha hizo haitaruhusiwa kuzitumia katika kufanya malipo popote duniani, na benki zote hazitaruhusiwa kulipa wala kupokea amana au maombi ya kubadilisha noti zilizoondolewa kwenye mzunguko"amesema ilulu
Ameongeza kuwa Benki kuu inatoa rai kwa wananchi wote wenye akiba ya noti hizo za zamani, kuzibadilisha au kuziweka kwenye benki yoyote ndani ya kipundi kilichotewa.
"Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya Mwaka 2006 sura ya 197 kifungu cha 26 kimeipa Benki Ku Mamlaka pekee ya kuchapisha notina kusambaza Nchini Tanzania huku kifungu cha 28(2) na (3) ya sheria hiyo Benki kuu imepewa mamlaka ya kusitisha uhalali ya fedha itakazozianisha kadri itakavyoona inafaa" amesema ilulu
Aidha amesema swala la uuzaji na kuuza sarafu haliko kisheria, ni kosa na sisi kama BOT haturuhusu.