MGOMBEA URAIS CHADEMA AISHIWA FEDHA ZA KAMPENI



Na Humphrey Shao

Ikiwa ni katika hatua ya awali ya mchakato wa Uchaguzi mkuu kwa wagombea urais wakiwa katika hatua ya kukusanya wadhamini nchi nzima, kwa upande wa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ameishiwa fedha za mafuta na Posho za wasaidizi. 

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizotufikia sauti ya Wananchi kutoka chanzo chetu cha uhakika zinaeleza  mpaka sasa Chadema hawana fedha za kuendeshea kampeni licha ya kuchukua ruzuku kwa kipindi cha miaka yote mitano.

Chanzo hicho kinasema Lissu ameunda kamati kadhaa za kukusanya fedha kutoka kwa marafiki na wafanyabiashara ili waweze kufanikiwa katika mchakato wa uchaguzi.

"Kama unavyotuona tupo hapa msimbazi kwa ajili ya kikao na mimi mmoja ya wanakamati wa kuchangisha fedha kwa ajili ya mgombea wetu wa Urais lakini hali ni mbaya kila tunayemgusa hayupo tayari kutusaidia wanasema tuachane na huu ujinga" kimesema chanzo chetu.

Amesema hali ya kiuchumi ya Chadema ni mbaya kwani Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe amegoma kutoa fedha kwa ajili ya shughuli za kampeni za mgombea urais.

“Kwasa  sasa zimeundwa kamati mbalimbali katika kanda tofauti kuhakikisha tunafanikisha hili, hali ya kifedha ndani ya chama si shwari na kila tunayemgusa anataka mahesabu ya Ruzuku na michango ya wabunge. 

Licha ya kamati hizi kuwepo maswali ya fedha za Ruzuku na michango ya wajumbe yamekuwa mengi kuliko kawaida maana wanachama wanataka kujua fedha ya chama chao ipo wapi,” kimeeleza chanzo hicho.

Aidha chanzo hicho kimesema jambo hilo linawapa wakati mgumu na kufanya wasifikie lengo na Mwenyekiti Mbowe kajiweka pembeni na hataki aulizwe juu ya fedha hizo.

Post a Comment

Previous Post Next Post